Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lakers wapo hoi, Golden State Warriors wadema NBA

NBA LEBRON Lebron James akiiifungia alama Lakers mbele ya wachezaji wa Portland

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Ligi ya kikapu chini Maremmani NBA imeendelea terna Alfajiri ya leo Februari 10, 2022 kwa michezo sita huku Los Angeles Lakers wakipokea kichapo cha sita kwenye michezo yake nane ya mwisho huku Golden State Warriors imesimamishwa kushinda mchezo wake wa kumi mfululizo baada ya kufungwa.

Lakers imefungwa na Portland Trail Blazers kwa alama 107-105 licha ya Lebron James kuwa nyota wa mchezo kwa kufunga alama nyingi zaidi, alama 30, rebound 7 na assist 7, Anfernee Simons akiwa mwiba mkali kwa lakers kwa kufunga alama 29 na assist 5 huku Anthony Davies akifunga alama 17, rebound 7 na assist 6.

Lakers sasa wamefungwa michezo 30 katika michezo 56 na kushika nafasi ya 9 kwa upande wa Ukanda wa Magharibi matokeo ambayo siyo mazuri kwa upande wao tena bila kuwa na nyota wao, Russell Westbrook, Carmelo Anthony na Deandre Howard.

Kwa upande mwingine, Golden State Warriors wamefungwa na Utah Jazz kwa lama 111-85 na kuvunjiwa ubabe wao wa ushindi katika michezo 9 mfululizo licha ya kusalia naffs ya pili kwenye mimano wa NBA ukanda wa Magharibi nyuma ya Phoenix Suns.

Warriors walicheza na nyota wake wakubwa wawili, Stephen Curry na Andrew Wiggins na kuwakosa wakina Klay Thompson na Dreymond Green jambo linalopelekea Curry kukosa msaada wa kutengenezewa nafasi nyingi za kufunga na hata akifunga basi anafunga alama chache, alama 16 tofauti na lama 30 na zaidi alizokuwa anafunga.

Michezo mingine ni, Cleveland Cavaliers 105-92 San Antonio Spurs, Charlotte Hornets 109-121 Chicago Bulls, Oklahoma City Thunder 98-117 Toronto Raptors na Sacramento Kings 132-119 Minnesota Timberwolves.

Chanzo: eatv.tv