Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lakers ndio mwisho wao ama? wapokea Kichapo cha tano NBA

James Le Nyota wa LA Lakers , Le Bron James

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

LA Lakers wamekumbwa na jinamizi gani kwenye NBA msimu huu? pengine ndilo swali unaloweza kujiuliza kwa sasa.

Lakers wamejikuta wakiambulia kipigo cha 5 kati ya michezo 7 waliyocheza hivi karibuni. Hali sio shwari pale Staple Centre msimu huu. Matokeo mabaya na uwepo wa majeruhi, ni miongoni mwa changamoto wanazopitia.

Wakiwa nyumbani dhidi ya Sacramento Kings, vigogo wa Los Angeles wameambulia kipigo cha pointi 141-137. LeBron James, Russell Westbrook na Anthony Davis kwa pamoja wamepachika pointi 82. Watamalizaje msimu huu?

Kwingineko kwenye NBA,

Stephen Curry ameiongoza Golden State Warriors kupata ushindi wa 10 wakiwa nyumbani. Warriors wameshinda kwa pointi 118-103 dhidi ya Portland Trail Blazers. Giannis Antetokounmpo ameiongoza Milwaukee Bucks kwenye ushindi wa pointi 120-109 dhidi ya Denver Nuggets.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live