Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

LA Lakers yavuliwa ubingwa, Booker awa gumzo NBA

BOOKER LA Lakers yavuliwa ubingwa, Booker awa gumzo NBA

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mabingwa watetezi wa ligi ya kikapu nchini Marekani NBA, Los Angeles Lakers wametolewa kwenye hatua ya robo fainali ya ligi hiyo kwa ukanda wa Magharibi na Phoenix Suns baada ya kufungwa kwa alama 113-100 Alfajiri ya kuamkia leo Juni 4, 2021.

Submitted by George David on Ijumaa , 4th Jun , 2021 Devin Booker wa Phoenix Suns (kulia) akijaribu kumpita Lebron James wa LA Lakers (katikati) kwenye mchezo wa NBA Playoff game 6 uliochezwa aalfajiri ya kuamkia leo na Suns kupata ushindi wa alama 113-100 na kufuzu nusu fainali kwa upande wa Magharibi.

Kipigo hiko kimewafanya Lakers kukubali kichapo cha nne katika michezo sita ya mtoano waliyocheza mfululizo na Phoenix Suns ilhali wakipata ushindi kwenye michezo miwili pekee ambayo haikutosha kuwabakiza kwenye michezo hiyo ya mtoano kuelekea Ubingwa wa NBA.

Jahazi la Lakers lilianza kuingia dosari baada nyota wake Anthony Davis kuzidi kupata maumivu ya nyonga na kushindwa kuendelea na mchezo na kutoka dakika tano tu baada ya mchezo kuanza hivyo kumfanya Devin Booker wa Suns kucheza kwa uhuru zaidi na kuwadhulu Lakers.

Hadi mchezo unamalizika, Booker ndiye aliyeibuka kuwa nyota kwa kufikisha alama 47, rebaundi 11 na assisti 3 na kumpiku mkali wa Lakers, Lebron James aliyeambulia alama 29,rebaundi 9 na assisti 7.

Nyota mwingine wa Suns aliyekuwa mwiba kwa Lakers ni Chris Paul ambaye ameweka rekodi ya kufikisha assisti 938 na kushika nafasi ya 15 kwa wachezaji wa NBA wa muda wote wenye assisti nyingi huku akiifikuza rekodi ya Kobe Bryant mwenye assisti 1,040 akishika nafasi ya 10.

Licha ya kutolewa kibabe lakini Lebron ameweka rekodi ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji wa NBA wenye kukinga zaidi mpira isiingie kwenye lango lake (blocking) nyingi kwa muda wote akishika nafasi ya kumi akiwa  na blocks 252 akiongozwa na Tim Duncan mwenye zaidi ya 500.

Lebron pia ambaye ametolewa kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa mtoano wa NBA, amesema sababu ya kuboronga msimu huu ni majeraha ambayo yaliwaandama wachezaji nyota kwenye kikosi hicho akiwemo Anthony Davis hivyo kikosi kukosa uwiano mzuri.

Mwisho Lebron akawavulia kofia Suns kwa kusema wamestahili kwasababu walikuwa na msimu bora na kukiri ubora wa Booker na kusema atafika mbali kwenye maisha yake ya NBA nchini Marekani.

Kwa upande mwingie, Wakali wa NBA kwa ukanda huo huo wa Magharibi, timu ya Denver Nuggets wamefuzu nusu fainali ya ukanda huo baada ya kuwashushia kipigo cha nne timu ya Portland Trail Blazers ya Carmelo Anthony baada ya jana kuibuka na ushindi wa alama 126-115.

Baada ya matokeo ya michezo hiyo, sasa Denver Nuggets watacheza na Phoenix Suns kwenye michezo ya nusu fainali ya NBA kwa ukanda wa Magharibi ilhali ukanda wa Mashariki, Brooklyn Nets watacheza na Milwaukee Bucks, Philadelphia 76ers na Atalanta  tarehe 6 Juni 2021.

Chanzo: eatv.tv