Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Kwa rekodi hii, Durrant hakamatiki NBA

DURRANT 1 Kevin Durrant (kulia)

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Kevin Durrant wa Brooklyn Nets ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 26 kufikisha alama 24, 007 kwenye historia ya NBA baada ya kukusanya alama 25, rebound 8 na Assits 4 zilizoisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa alama 104-90 dhidi ya Washington Wizard alfajiri ya leo Oktoba 26, 2021.

Kwa alama hizo 24, 007, Durrant anashika nafasi ya tatu kwa wachezaji wenye alama nyingi kwa wale wanaoendelea kucheza mpaka hivi sasa nyuma ya Carmelo Anthony mwenye alama 27, 423 na kinara Lebron James wawili hawa wa LA Lakers huku James akiwa na alama 35, 445.

Durrant sasa anasaka alama 361 kuifikia nafasi ya 25 ya Gwiji wa zamani wa Philadelphia 76ers, Allen Iverson mwenye alama 24, 368.

Chanzo: eatv.tv