Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Klay Thompson kucheza NBA G league

KLAY THOMSON Klay Thompson kucheza NBA G league

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Mchezaji wa Golden States Warriors, Klay Thompson amejiunga na timu shirikishi ya Santa Cruz Warriors iliyopo NBA G League, ilikupata utimamu wa mwili baada ya kuchanika misuli msimu wa mwaka 2019/2020.

Akiwa hajacheza mchezo hata mmoja wa msimu uliopita, Thompson anajiunga na Santa Cruz ikiwa ni sheria ya NBA kumtaka mchezaji aliyepata majeraha yaliyohatalisha urejeo wake ndani ya ligi hiyo, kujiunga na G League ilikurudi kwenye hali ya ushindani.

Thompson ameshindi taji la NBA inayofahamika kama Larry O'brien Trophy, mara akiwa na Golden States warriors na msimu huu timu hiyo inatazamiwa kushinda kombe hilo baada ya kushinda mechi 18 na kufungwa mbili pekee.

Kwa sasa, Thompson ataendelea na kujifua ndani ya G-League pamoja na Wiseman na wachezaji wengine wa Santa Cruz. Bado haijafahamika wazi ni lini Thompson atachukua nafasi hiyo ndani ya Santa Cruz, lakini anaonekana kuwa karibu zaidi ndani ya GSW.

Chanzo: eatv.tv