Kareem Abdul-Jabbar hakuwa shabiki wa aina ya ushangliaji wa LeBron James wiki iliyopita wakati nyota huyo wa NBA alipowasaidia Los Angeles Lakers kuwashinda Indiana Pacers.
Ilikuwa moja ya michezo wa mwisho kwa James kabla ya kuwekwa kwenye itifaki za afya na usalama za NBA baada ya kukutwa na virusi vya UVIKO-19. James baadaye alibainika kutokuwa na Corona, ripoti ambayo ilimruhusu kurudi kwenye mechi zinazofuata.
Katika ushindi dhidi ya Pacers, James alipigwa faini ya dola za Kimarekani $15,000 sawa na Shilingi za Kitanzania 34,530,000 baada ya kuwakejeli mashabiki wa Indana kwa aina yake ya ushangiliaji.
Abdul-Jabbar alisema mtu kama James hapaswi kufanya aina hizo za ushangiliaji. "Kwangu mimi, kushinda kunatosha. Kwa nini unahitaji kufanya densi ya kukejeli, ya kitoto na kutoheshimu timu nyingine kwenye korti? ," alisema mkongwe huyo wa NBA.
Lakers msimu huu inaundwa na kundi la wachezaji wakongwe ambao bado wanapaswa kuzoea aina ya uchezaji wa kila mmoja wao. Pia mabingwa hao wa mwaka 2020 wamekuwa wakipata shida kwenye upatikanaji wa ushindi pindi LeBron anapokosekana kiwanjani.
Mpaka sasa Los Angeles imeshinda 12 na kufungwa 12 na wameketi katika nafasi ya 8 katika Msimamo wa Magharibi mbele ya Dallas Mavericks, Denver Nuggets, Minnesota Timberwolves na Portland Trail Blazers.