Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Huyu Jesca kawa mtamu balaa

Jesca+pic Huyu Jesca kawa mtamu balaa

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIVER ALBERT NYOTA njema huonekana asubuhi. Ndivyo unavyoweza kusema kwa Jesca Ngisaise ambaye ameweka rekodi kabambe kwenye mpira wa kikapu hapa nchini.

Jesca mwenye umri wa miaka 17 ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga pointi nyingi katika mchezo mmoja na hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo nchini iwe kwa wanaume au wanawake katika historia ya mchezo huo.

Mchezaji huyo mrefu kiasi alifunga pointi 105 timu yake ya JKT Stars ilipoichapa Ukonga Princess pointi 166-7 katika mechi ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), iliyofanyika Agosti 22, mwaka huu.

Achana na rekodi hiyo, pia ndiye anayeongoza kwa kufunga pointi nyingi ligi ya RBA upande wa wanawake akifunga pointi 229, akifuatiwa na Faraja Malaki wa Jeshi Stars mwenye nazo 105.

Vilevile ndiye mchezaji anayeongoza kufunga kwa mitupo mitatu (three points) akifunga mara 28, akifuatiwa na Faraja aliyefunga mara tisa.

Pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya wanawake na aliwahi kwenda Afrika Kusini 2017 alikoshiriki mafunzo ya mchezo huo yaliyoendeshwa na makocha wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), maarufu Basketball Without Borders.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz