Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Golden State na Chicago Bulls zaonja vipigo NBA

Hh.jpeg Kikosi cha Golden State Warriors dimbani

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya Golden State Warriors imekutana na kipigo cha kwanza katika msimu mpya wa NBA baada ya kupoteza dhidi ya Memphis Grizzlies kwa alama 104-101.

Grizzlies ilisota kwa alama 19 nyuma katika robo ya pili lakini Jo Morant ambaye alifunga alama 30 alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwapa kipigo cha kwanza Golden State Warriors baada ya kushinda mechi nne mfululizo.

Stephen Curry alimaliza mchezo akiwa ndiye mfungaji bora wa akimaliza na alama 36, ingawa alishindwa kuisaidia Golden State Warriors kuepuka kipigo.

Timu nyingine ambayo ilianza msimu vizuri ni Chicago Bulls ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya New York Kniocks kwa alama 104-103.

Knicks iliongoza kwa alama 104-91 zikiwa zimesalia dakika tatu katika robo ya nne kabla ya mchezo kumalizika lakini wakairuhusu Bulls kufunga alama 92 bila majibu na wakakaribia kushinda mchezo.

DeMar DeRozan alikosa mtupo huru ambao ungeipa ushindi Bulls dakika za mwisho lakini hali ikawa tofauti huku Kemba Walker alifunga alama 21 kwa upande wa Knicks naye RJ Barret alifunga alama 20.

Chanzo: eatv.tv