Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Golden State gari limewaka NBA

Golden State (600 X 729) Golden State waendeleza rekodi ya ushindi NBA

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golden State Warriors, ndio timu yenye rekodi bora NBA mpaka sasa, ingawa kwa walio wengi haikutarajiwa kufanya hivyo

Warriors wameimarisha rekodi yao leo kwa kushinda mchezo wa 10 kwa kuwapiga Minnesota Timberwolves kwa vikapu 123 - 110.

Andrew Wiggins, ameweka points 35 leo kwa Warriors katika mchezo wa kuvutia mno na mpaka sasa Warriors wamepoteza mchezo mmoja tu

Katika michezo mingine

Kevin Durant "KD" bado yuko kwenye moto na leo amewaongoza Brooklyn Nets kuwamaliza Orland Magic kwa points 123 - 90 ambapo KD ameweka points 30 katika hizo.

Lakini mchezaji LaMarcus Aldridge ambae amerudi mchezoni hivi karibuni baada ya kutangaza kustaafu msimu ulipopita kutokana na matatizo ya Moyo ameng'ara pia leo hii.

Aldridge amepiga points 21 kwa Nets katika ushindi huo wa leo.

Lakers ilibidi wasubirI muda wa nyongeza kama ilivokua mchezo uliopita ili kuwapiga Miami Heat, wakashinda kwa points 120 kwa 117.

Muda wa kawaidia uliisha wakiwa 112 - 112 na ndipo zilipoongezwa dakika na lakers kupata ushindi huo.

Russell Westbrook alipiga triple double za points 25, Rebounds 12 na Asisst 14 katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live