Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Golden State Warrirors wapata pigo kubwa

CURRY 1 Golden State Warrirors wapata pigo kubwa

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya Golden State Warriros ya ligi kuu ya kikapu nchini Marekani, imepata pigo kubwa baada ya mchezaji wake nyota, Stephen Curry kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki moja nyingine baada ya vipimo vya MRI kuonesha kuwa nyota huyo ameathiriwa zaidi kwenye nyonga yake

Submitted by George David on Jumatano , 24th Mar , 2021



Stephen Curry akiinuliwa baada ya kudondoka chini.

Curry alipata majeraha hayo wiki iliyopita baada ya kupewa kikumbo na mlinzi wa timu ya Houston Rockets kilichomfanya ayumbe na kudondokea kwenye ngazi na kushindwa kuendelea na mchezo huo ikiwa ni ungwe ya tatu ya mchezo.

Mpaka hivi sasa Curry ameshakosa michezo miwili ya timu yake ikiwemo kipigo cha alfajiri ya leo dhidi ya Philadelphia 76ers kwa alama 109 kwa 98. Hii ni mara ya tatu Curry kupata majeraha katika misimu mitatu mfululizo.

Chanzo: eatv.tv