Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Golden State Warriors yakwaa kisiki |

Ja 1 Golden State Warriors yakwaa kisiki |

Sat, 22 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Memphis Grizzlies imefuzu kucheza mtoano kwenye Ligi ya Kikapu nchini Marekani baada ya kuifunga Golden State Wariors katika muda wa nyiongeza kwa alama 117-112.

Ja Morant mwenye umri wa miaka 21, aliifungia Grizzlies alama 35 zikiwemo alama nne za mitupo miwili ndani ya sekunde nne zilizokuwa zimesalia kumalizika mchezo, huku Stephen Curry akiifungia Warriors alama 39 katika mchezo huo.

Inakuwa ni kwa mara ya kwanza Grizzlies inafuzu hatua ya mtoano ya NBA katika misimu minne mfululizo.

Grizzlies itacheza mchezo wa kwanza wa mtoano katika ukanda wa Magharibi dhidi ya Utah Jazz mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili.

Michezo mingine ya mtoano itazikutanisha Milwaukee Bucks dhidi ya Miami Heat (Mashariki),LA Clippers watamenyana na Dallas Mavericks (Magharibi) michezo yote itaanza siku ya Jumamosi.

Chanzo: eatv.tv