Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Doc Rivers aweka rekodi ya kibabe NBA

DOC RIVERS 1 Doc Rivers aweka rekodi ya kibabe NBA

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Kocha wa Philadelphier 76ers, Doc Rivers ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kumi kwenye historia ya Ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA' baada ya kuifunga Chicago Bulls kwa alama 114-105 alfajiri ya kuamkia leo na kufikisha ushindi wake wa 1,000 ndani ya misimu 23 aliyokuwepo NBA.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Rivers alielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kukutana wachezaji wake wakimoigia makofi ya hongera na ghafla nyota wa timu hiyo, Joel Embiid alimeagia mabarafu na maji kama eneo la shangwe.

Rivers amabye ametimiza miaka 60 Oktoba 13 mwaka huu, amesema, “Sikuwaza kama nilikuwa na ushindi wa 999. Sikuwa nimehesabu. Sio kitu ambacho huwa nafanya lakini ushindi huo kutokea Chicago unamaana kubwa sana. Na pia ina maanisha nina bahati sana”

“Vijana walijipanga vizuri kuifanya hii surprise. Ilikuwa baridi sana. Natamani ingekuwa bia” akaeleza Doc Rivers.

Rivers kwa sasa amefikisha ushindi wa 1,000 na kupoteza michezo 706 kwenye misimu 23 aliyofundisha timu za Orlando Magic, Boston Celtics, Los Angeles Clippers na sasa Philadelphia 76ers.

Kwenye orodha ya makocha wenye ushindi katika michezo mingi kwenye historia ya NBA ni kinara Don Nelson mwenye ushindi 1,335 wakati Gregg Popovich ambayo ni kocha wa timu ya San Antonio Spurs kwasasa na timu ya taifa ya Marekani ya Mpira wa kikapu ana ushindi 1,313.

Chanzo: eatv.tv