Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

DeRozan aibeba Chicago Bulls NBA

DEROZAN DeRozan aibeba Chicago Bulls NBA

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

DeMar DeRozan ameiongoza Chicago bulls asubuhi ya leo kwa kuilaza Boston Celtics kwa alama 128-114 ambapo, DeRozan alifunga pointi 37, na kuwa nyota wa mchezo kwa mara ya pili mfululizo huku Zach LaVine alikuwa na pointi 26 na asisti saba, na kuingoza Bulls kushinda.

Boston Celtics waliongoza kwa pointi 19 mwishoni mwa robo ya tatu kabla ya Bulls kujibu mapigo kwa 29-9 kati ya vipindi na kuchukua uongozi wa 106-105 kupitia Ayo Dosunmu kwa pointi tatu zikisalia dakika 6:54. Chicago Bulls iliishinda Boston 39-11 kwa jumla katika robo ya mwisho.

Dosunmu alimaliza akiwa na pointi 14, Lonzo Ball aliongeza 12 naye Nikola Vucevic akafikisha pointi 11, rebounds 10 na asisti tisa kwa Bulls, ambao walipata ushindi wao wa sita katika michezo saba ya kufungua msimu.

Jaylen Brown alikuwa na pointi 28 na rebounds saba akiongoza Celtics. Jayson Tatum alifunga pointi 20, Al Horford akafunga 20 na rebounds 10, na Marcus Smart alifunga 16 kwa Boston. Smart baadaye aliwakosoa Brown na Tatum kwa kutopasisha mpira vya kutosha.

Boston ilishuka hadi 2-5, ikiashiria mwanzo mbaya zaidi wa mechi saba tangu kuanza kampeni ya 2006-07 na kupoteza sita katika michezo saba.

Chanzo: eatv.tv