Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Curry na Bridges bora NBA Week 1

NBA WEEK 1 Curry na Bridges bora NBA Week 1

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Wiki ya kwanza ya Ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA' imemalizika, na wasimamizi wa ligi hiyo imewatangaza Stephen Curry wa Golden State Warriors na Miles Bridges wa Charlotte Hornets kuwa wachezaji bora wa wiki hiyo baada ya kuonesha viwango bora zaidi.

Submitted by George David on Jumanne , 26th Oct , 2021 Stephen Curry wa Golden State Warriors (kulia) na Miles Bridges (kushoto) wa Charlotte Hornets.

Stephen Curry alianza kwa moto mkali baada ya kupiga 'Tripple Double' dhidi ya Los Angeles Lakers, alama 21, rebound 10 na Assist 10 na kuendeleza kiwango hiko na kuna na wastani mzuri wa kufikisha alama 31.0, rebound 9.0 na Assist 7.0 na kuisaidia Golden kushinda michezo 3 mfululizo.

Miles Bridges wa Charlotte Hornets alikuwa na wastani wa alama 25.0, rebound 8.0 na Assist 2.0 na kuisaidia timu yake kushinda michezo 3 mfululizo na kuwa sehemu kubwa ya kutegemewa kwenye timu hiyo.

Chanzo: eatv.tv