Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Clippers kuanza na Timberwolves April 12

Timberwolves Clippers kuanza na Timberwolves

Fri, 8 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Los Angeles Clippers wanatarajia kucheza dhidi ya Minnesota Timberwolves siku ya April 12, kwenye mchezo wa hatua ya awali kupambania nafasi ya kuingia nane bora katika mbio za ubingwa wa NBA ukanda wa magharibi. 

Clippers wamefanikiwa kushika nafasi ya nane kwenye misimamo wa ligi ukanda wa magharibi baada ya kuifunga New Orleans Pelicans huku washindani wao Timberwolves waliifunga Denver Nuggets na kumaliza nafasi ya saba ambapo mshindi wa mechi ataungana na atakayeshinda mtanange wa  Pelicans dhidi ya San Antonio Spurs walioamliza nafasi ya tisa na kumi.

Kawhi Leonard anatazamiwa kurejea kwa upande wa Clippers walioifunga Timberwolves, mara tatu msimu huu na kupoteza mara moja, Paul George akianza mechi tatu na kukaa benchi kwenye mechi ambayo walipoteza.

 

Chanzo: eatv.tv