Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Chicago Bulls yazidi kuiangamiza LA Lakers

Lebron James Lebron James wa Lakers akiwa anajaribu kufunga mbele ya mlinzi wa Chicago Bulls

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Los Angeles Lakers wameendelea kususua kwenye msimu huu wa NBA mwaka 2021-22 baada ya kupokea kipigo cha kingine cha alama 121-103 kutoka kwa Chicago Bulls Alfajiri ya leo.

Lakers wamekuwa wakifanya vibaya tangu LeBron James apate majeraha msimu huu, na kumpelekea kocha Frank Vogel kubadilisha kikosi kila siku hii ni kutokana na kukosa muunganiko na wachezaji sahihi wakumpa matokeo licha ya kuwa na lundo la wachezaji nyota.

Alama 20 pamoja na ribaundi 6 za Anthony Davis hazikutosha kuipa ushindi Lakers waliodhofu bin hali mbele ya vijana wa Chicago Bulls, wanaongozwa na DeMar DeRozen ambaye aliyefunga pointi 38 na assisti 6 .

Alex Caruso aliyehudu ndani ya Lakers msimu uliopita na sasa akiwa na Chicago, alicheza dakikia 34 bila kufunga alama yoyote licha ya kutoa assisti 6 na riboundi 5.

Chanzo: eatv.tv