Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Ben Simmons hoi, akabiliwa na ukata

Simmons Ben huenda akarudi uwanjani ili kukabiliana na ukata

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali si shwari kwa mchezaji wa timu ya Philadelphia 76ers katika ligi ya kikapu ya NBA, Ben Simmons ambae amegoma kuichezea timu yake mpaka sasa.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari Ben Simmons ameripotiwa kuishiwa hela kwa sasa kutokana na faini anazopigwa na timu yake ambazo ni kubwa kwa sababu ya kugomea kucheza timu hiyo huku akiwa bado na mkataba nao.

Ukiachilia faini ambazo amekua akipigwa pia Ben Simmons anedaiwa kutumia vibaya mno mapato yake ikiwemo kununua gari mpya kila mwezi na starehe nyengine jambo ambalo linamfilisi wakati huu.

Simmons amegoma kuchezea timu yake hiyo tangu walipotolewa kwenye hatua ya mtoano msimu uliopita huku Simmons akilaumiwa kua ni mchezaji aliyekua chini ya kiwango na akishindwa kuisaidia timu yake katika nyakati muhimu.

Simmons ameshutumiwa mara kadhaa na wachambuzi pamoja mashabiki kutokana na jinsi anavyoigharimu timu mchezoni ndipo aliposusia hatua zote kuanzia mazoezi hadi mwanzo wa ligi na mpaka sasa hajashiriki katika mchezo wowote akisema hayuko sawa kiakili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live