Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Anthony Davis na Lakers wapata majanga NBA

AD INJURY Anthony Davis na Lakers wapata majanga NBA

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Imefahamika kuwa, sababu ya nyota wa Los Angeles Lakers, Anthony Davis kutorejea uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Portland Trail Blazers alfajiri ya kuamkia Jumapili ya Novemba 7, 2021 ni kwasababu aliumia kidole gumba cha mkono wa kulia na kuumwa tumbo.

Davis aliambulia kucheza dakika 7 pekee na kukusanya alama 2, rebound 3 bila kutoa assist baada ya kupata majanga hayo yaliyompelekea atolewe uwanjani na kushindwa kurejea na timu yake ya Lakers kufungwa kwa alama 105-90 dhidi ya Portland Trail Blazers.

Kipigo hicho kwa Lakers ni majnaga mengine, kwani wamerekodi kipigo chao cha tano kwenye michezo yao kumi ya mwanzo kwenye msimu huu mpya wa NBA wa mwaka 2021-2022 ilhali kikiwa ni kipigo cha 11 katika michezo yake 16 kwa kujumuisha na vipigo 6 mfululizo vya NBA Pre-Season.  

Chanzo: eatv.tv