Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu atamba kuwakalisha wasanii wote wa kike Afrika

Zuchu .png Zuchu

Sun, 3 Apr 2022 Chanzo: dar24.com

Mwanamuziki mahiri kutoka WCB, Zuhura Othman maarufu, Zuchu amejinadi katika mtandao wa Twitter na kutamba kuwa yeye ndio msanii pekee wa kike anayelipwa zaidi kutoka ukanda wa nchi za AfrIka mashariki kwa sasa.

Zuchu amewaahidi mashabiki zake kuwa ndani ya mwaka huu wa 2022, atatoa album yake ya kwanza hivyo amewataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kupokea burudani zaidi kutoka kwake.

“I’am forever grateful to my fans, y’all just made me the most paid female artist in East Africa, I love y’all, Promising you an album this year, you deserve it, get ready ypu bout to take of,” amenukuliwa Zuchu kitoka Twitter.

Mwanamuziki huyo kwa sasa anafanya vizuri kupitia kibao ‘Mtasubiri’ alichoshirikishwa na kiongozi wake Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz, kibao kinachopatika kwenye Extended Playlist (EP) mpya ya Diamond.

Chanzo: dar24.com