Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Morogoro Jazz Band Rtd Dar Es Salaam Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz, bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM, bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi, Shemeji, Bujumbura, Ilikuwa lifti, Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki, Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga, Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri, Beno Villa Anthony, Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi', Suleiman Mbwembwe, Shaban Dogodogo, Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live