Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizkid amnunulia gari la thamani meneja wake

Wizzz Wizkid

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: dar24.com

Mshindi wa tuzo ya Grammy mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Ayo Balogun maarufu Wizkid amempatia zawadi ya gari  aina ya SUV Toyota Prado meneja wake aitwaye Sunday Are.

Meneja huyo amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Wizkid tangu mwaka 2015 ambapo tangu wameanza kufanya kazi pamoja mwendendo wa kazi na mafanikio ya msanii huyo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa siku baada ya siku.

Sunday ameweka kipande cha video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kikimuonyesha akiwa mwenye furaha sana,huku akiiambatanisha na maneno machache yaliyosomeka.

“What a way to start the new week, another surprise from @wizkidayo himself, can’t thank you enough”

Sunday Are ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kusimamia wasanii wa muziki nchini Nigeria iitwayo ‘List Entertainment Company’ ambayo imewahi kuwasimamia wasanii wengine nyota kama Asa, Lagbaaja, Majek Fashek na wengine kadhaa.

Chanzo: dar24.com