Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizkid aacha historia Madison Square Garden (+Video)

Wiz Kid Ayo Wizkid

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Nigeria, wizkidayo siku ya jana ameujaza uwanja wa Madison Square Garden jijini New York City ukumbi huu maarufu zaidi Duniani, wenye uwezo wa kuingiza watu 20,789.

Wizkid anajibu mapigo ya Burna Boy ambae mapema mwaka Huu aliijaza Madison Square Garden.

Wasanii wanaotoka ukanda wa Africa, Wizkidayo na Burna Boy pekee wanaingia kwenye historia ya kuujaza Ukumbi huu.

Lakini Pia Wizkid anaingia kwenye list ya Mastaa wakubwa duniani ambao waliwahi kuujaza uwanja huu ambao unaoingiza Maelfu ya watu, akiwemo Jay-Z, Justin Bieber, Michael Jackson, Elvis Presley, The Beatles, Adele, pamoja na Rihanna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live