Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Wasi wasi" wachelewesha Albamu ya Cardi B

Cardi B Rapa Cardi B

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Cardi B ameingiwa na hofu, na hiyo ndio sababu kuu ambayo inamfanya achelewe kuachia Album mpya kwa kipindi cha miaka mitatu sasa. Cardi B anasema amekuwa muoga kuachia ngoma kutokana na watu kumkosoa sana.

“Kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 nilikuwa napenda Muziki, lakini kwa sasa, kufanya muziki kwangu mimi imekuwa Kazi ambayo inanifanya niwe na wasiwasi.

Kwa sababu kila mmoja anakosoa kila kitu ninachofanya. Wakati mwingine hupaswi kufanya kitu ambacho kinakufanya uwe na wasiwasi.” alisema Cardi B.

Tangu alipoachia Album yake ‘Invasion of Privacy’ mwaka 2018, Cardi B amekuwa akirekodi nyimbo lakini haridhishwi na anachokifanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live