Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii waomba punguzo maeneo ya vivutio vya utalii

WhatsApp Image 2022 12 16 At 13.jpeg Wasanii waomba punguzo maeneo ya vivutio vya utalii

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: Michuzi

Wasanii wa filamu nchini wametembelea vivutio vya utalii vilivyopo Moshi mkoani Kilimanjaro huku wakiomba kuwepo na vibali vyenye gharama nafuu ili wazalishe kazi nyingi ndani ya vivutio hivyo.

Akizungumza na Michuzi Blog leo Desemba 16 baada ya kutembelea vivutio hivyo vya utaliii ikiwa ni sehemu ya Royal Tour, Msanii mkongwe nchini Abdulaziz Babu amesema ni jukumu la wasanii kuendeleleza kazi iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha watalii nchini.

"Mama yetu Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watalii wanafika nchini Tanzania kuona vivutio vilivyopo , hivyo wasanii ni kazi kwao kuendeleza juhudi hizo kupitia tamthilia na Filamu wanazozalisha walau kuwepo kwa vipande vinavyoonyesha utalii wetu ikiwemo Misitu,uoto wa asili pamoja na mandhari ya maeneo ya misituni."

Babu amewaomba nafasi hiyo kuwaomba wasimamizi wa vivutio hivyo kuweka bei rafiki kwa vibali vya wasanii kuyatumia maeneo ya hifadhi ya utalii ili kuwepo kwa watayarishaji wengi kufika katika hifadhi mbalimbali nchini katika kutangaza vivutio vya utalii.

Kwa upande wake Mkongwe wa Tasnia ya Filamu Ahmed Olotu maarufu Mzee Chilo amesema kupitia Bodi ya Filamu imempa fursa kama Msanii kutembelea kando kando ya Hifadhi ya Mlimani Kilimanjaro.

"Tunaona umuhimu wa kuwa na tuzo hizi sio tu ushindani bali wasanii wamepata fursa ya kuongeza ujuzi kwa maeneo mengi (Location) ya kutengeneza kazi zao hivyo kiukwei tumepata hamasa kubwa sasa hususani kwa watayarishaji kutengeneza kazi ndani ya vivutio vya utalii. "

Wakati huo huo muigizaji Neema Walele a.k.a Brenda ametoa ahadi ya kuwa mtayarishaji wa kwanza kufika Hifadhi ya pembezoni mwa Mlimani Kilimanjaro kutengeneza filamu yake mwakani.

"Tumekuwa na dhana ya kuamini kuwa kuna ugumu katika kufika katika vivutio vya utalii lakini niwatoe hofu wadau wa Filamu kutengeneza kazi zao katika vivutio vya utalii na kufata masharti na kulipia vibali haiwezekani wageni waje nyumbani kwako watumie vitu vyako ambavyo wewe mwenye huvipi kipaumbele kuvitumi.

"Sasa ni wakati wetu wasanii kutumia vivutio vyetu kwenye filamu zetu ambazo hata zikifika kwenye soko la Kimataifa tutakuwa tunaendelea kutangaza upekee wetu uliopo nchini Tanzania. "

Wasanii wamepata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro,Maporomoko ya Maji yaliyopo Materuni pamoja Msitu wa Rau uliopo Moshi Mkoan Kilimanjaro.

Chanzo: Michuzi