Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii kupokea asilia 70% mirabaha

COSOTA Wasanii kupokea asilia 70% mirabaha

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: millardAyo

Wakati Wasanii wa Tanzania wakisubiria kuanza kulipwa kutokana na kazi zao kutumika sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye TV, Radio na maeneo mengine yanayotumia muziki kuanzia December 2021, Afisa TEHAMA wa COSOTA amesema mgao wa pesa Wasanii watapata 70% na Serikali ni 30%.

"Mgao wa pesa ni kwamba Msanii atapata asilimia 70 na COSOTA inapata asilimia thelathini, tutapokua tunakusanya hizi pesa hazitokuwa zinakwenda kwenye masurufu mengine Serikalini ndio maana imekua 70% tunawapa wao na 30% tunatumia sisi kwa matumizi ya kuturahisishia kufikia maeneo mbalimbali kuwakusanyia wao pesa wanayotakiwa kuipata"

“COSOTA tumeandaa mfumo utarahisisha sana zoezi la ukusanyaji mirabaha kwani Msanii atakua na uwezo wa kupata mirabaha yake kwa namna pana zaidi kwasababu Halmashauri zinazokata leseni za biashara zitakuwa na uwezo wa kuwaomba Wafanyabiashara pia kuingia kwenye website na kulipia leseni za biashara zao na kulipia leseni za matumizi ya kazi za muziki moja kwa moja kwenye madawati yao na hawatokua na ulazima wa kuja COSOTA”

"Wataingia kwenye www.hakimiliki.co.tz wataweka taarifa zao za biashara na kupata control number na kulipia leseni yake ya matumizi ya kazi za muziki, tumefanya kikao na kuwaelimisha Maafisa Utamaduni na Maafisa Biashara ili wawape elimu hiyo Wafanyabiashara ili kuondoa usumbufu na mlolongo usiohitajika" , amesema Afisa TEHAMA Mwandamizi COSOTA Segenge James.

Chanzo: millardAyo