Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walikuwa washkaji sana tu, ila ghafla!

Diamond Pic Data (600 X 450) Diamond na Ommy Dimpoz, walikuwa washkaji ila kwa sasa sio marafiki kabisa

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Bongo Fleva ni muziki ambao wasanii wana ushirikino mkubwa katika kufanya kazi ya kuburudisha mashabiki. Katikati ya burudani hiyo ndio sehemu ya kunufaika na kazi yao na kupata fursa nyingine lukuki.

Makala haya inazungumzia nyota kizazi kipya waliokuwa na uhusiano mzuri hadi kufikia kufanya kazi pamoja, lakini ghafla wamegeuka kuwa maadui au unaweza kusema kuwa ilikuwa poa tu ghafla mkwanja ukaleta makuu’ huu ni mstari wa moja la shairi la wimbo wa Mwana FA uitwao Asanteni kwa Kuja.

DIAMOND NA DIMPOZ

Hawa ni mfano mzuri kwenye hilo. Mwanzoni kabisa walikuwa wanashibana kimuziki hadi kukutana kwenye kolabo tatu zenye uzito lakini sasa ni paka na panya.

Hakuna ubishi kila mmoja ana heshima yake katika muziki na kila mmoja ana ngome anayoiwakilisha. Mara ya kwanza walikutana kwenye wimbo wa Dully Sykes uliokwenda kwa jina la ‘Utamu’, kazi hii iliwakutanisha watu wenye ujuzi wa kucheza na sauti na ndio sababu hata wimbo huu ulifanya vizuri.

Baada ya ngoma hiyo, waka- kutana tena kwenye remix ya wimbo wa ‘Piga simu’ wa Diva. Mara ya kwanza Diva aliufanya wimbo huu na Diamond na ulifanya vizuri. Safari yao ya mwisho katika kolabo ni pale walipopewa shavu na Victoria Kimani wa Kenya kwenye wimbo wa ‘Prokoto’ uliofanya vizuri kimataifa na kufungua milango kwa wasanii hawa.

Licha ya kulabo hizo, wasanii hawa walikuwa miongoni mwa wale waliounda kundi la Kigoma All Stars na pia walisikika kwenye ngoma mbili za kundi hilo - Leka Dutigite na Nyumbani.

Hata hivyo, kwa sasa Diamond na Dimpoz hawana ukaribu wa kikazi na walishawahi kuingia kwenye vita ya maneno mtandaoni.

Ommy kwa sasa ana ukaribu mkubwa wa kikazi na Alikiba ambaye anatajwa kuwa hasimu mkubwa Diamond kimuziki.

Lakini Ommy asingemjua Diamond bila Alikiba,kupitia wimbo Nai Nai ndipo Dimpoz alitoka na kufahamika. Ulikuwa ni wimbo wa kwanza kwa msanii huyo kutoa akiwa kama msanii chipukizi kutokana na ukubwa wa jina la Alikiba na uwezo alioonyesha katika wimbo huo ulimfanya Dimpoz kuteka miji.

ALIKIBA NA BARAKA

Wasanii hao walikuwa na ukaribu hadi kufanya wimbo pamoja uliokwenda kwa jina la ‘Nisamehe’ ambao ulipokewa vizuri na mashabiki wa kazi za Alikiba na kumtambulisha zaidi Baraka.

Wawili hao walionekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja na baadaye waliingia kwenye lebo moja iliyofahamika kwa jina la RockStar Afrika na baada ya ugomvi wao ambao haikujulikana ni nini Baraka alijitoa na kuendelea na maisha mengine.

Baada ya kujitoa Kiba alibaki mwenyewe hadi alipoingia Dimpoz na ambaye kwa sasa kabaki mwenyewe kwenye lebo hiyo baada ya Kiba kujitoa na kuanzisha lebo yake inayojulikana kama King Music. Kiba kwenye lebo hiyo pia tayari amewapoteza nyota wawili ambao walijitoa na kwenda kujaribu sehemu nyingine - wapo Konde Gang ambao ni Cheed na Killy baada ya kufanya kolabo kadhaa na Aliba.

TEMBA NA CHEGE

Wakongwe hao wenye walijibebea umaarufu mkubwa nchini hasa Temeke kutokana na kuanzisha kundi pamoja na kulipa jina TMK Family walikuwa pamoja kwa muda mrefu na kufanikiwa kujizolea umaarufu, sambamba na mafanikio mbalimbali wameimba nyimbo nyingi pamoja na Wanaume.

Wawili hao kwasasa wanadaiwa hawana maelewano kiasi kwamba Chege aliamua kujitoa kwenye kundi na kuamua kuendesha maisha yake ya muziki akiwa amesimama mwenyewe.

BOB JUNIOR NA DIAMOND

Bob Junior ni msanii na mwandaaji wa kazi za wasanii. Ni maarufu sana kutokana na ujuzi wake huo. Upande wake ameingia kwenye makala hii kama mwandaaji aliyemtoa Diamond alipokuwa anaingia kwenye tasnia hiyo.

Bila huyo huenda hakuna mtu ambaye angemfahamu nyota wa burudani kwa sasa Diamond. Ndiye aliyemuandalia kazi kama Ntarejea, Nenda Kamwambie ambazo ni miongoni mwa zilizomtambulisha msanii huyo.

Wawili hao kwa sasa hawana maelewano kwani kila mmoja anaendelea na maisha yake, chanzo cha ugomvi wao wanajua wenyewe.

Chanzo: Mwanaspoti