Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: ‘Nibadilishe’ wa Goodluck Gozbert unaonyesha maisha ya watu wengi

Video Archive
Thu, 29 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Tanzania, Goodluck Gozbert amesema alichoonyesha kwenye wimbo ‘Nibadilishe’ ndiyo maisha halisi ya watu wengi.

Amesema wengi wanafahamu Biblia na wanaamini Mungu yupo, lakini wanakwama kubadilika kutokana na sababu wasizozijua.

“Nilifanya tafiti yangu ndogo kwa kuzungumza na watu wakiwamo vijana, wengi walinijibu kuwa wanatamani kubadilika, lakini wanashindwa na kuishia kudanganya mbele ya viongozi wa dini.”

“Wapo ambao wakienda kuzika wanaposikia mahubiri, hujiapiza kubadilika, lakini wakitoka hapo wanarudia yaleyale,” amesema Gozbert.

Kuhusu maudhui ya wimbo huo uliotoka hivi karibuni, amesema watumishi  wa Mungu wanapata ujumbe ukiwa na maudhui ya kuzungumza kitu fulani, lakini  namna ya kukiwakilisha inakuwa tofauti.

“Mimi kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu na ninaimba, nikipata ujumbe ninaufanyia kazi kulingana na kipaji changu.”

Pia Soma

Mwimbaji huyo amesema, “hata huu ulikuwa ujumbe wa Mungu kwangu, nikaufanyia kazi kwa kupata maoni ya watu, kabla ya kuandika wimbo na hatimaye kufikisha ujumbe husika.”

Ameeleza wimbo huo ameutoa wakati huu kwa sababu ni wakati wa Mungu,“alinipa ujumbe wakati huu niimbe kuhusu hilo, nimefanya na nina imani utaokoa na kuimarisha imani za walio wengi.”

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz