Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukaribu wa Kiba, Maua Gumzo

Kiba Maua Ukaribu wa Kiba, Maua Gumzo

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukaribu wa mastaa wawili wakubwa wa Bongo Fleva, King Kiba na Maua Sama umeibua gumzo kama lote. Walianza kwa kusambaa kwa picha yao ya pamoja kabla ya Maua kwenda kufanya shoo ya kiwango kwenye ziara ya kimuziki ya Kiba jijini Mwanza.

Hata hivyo, ming’ono imezidi baada ya King Kiba kumjibu Maua Sama kwa kumwambia hakuna mtu wa kumpiga akirudia kusikiliza wimbo wake wa Zai, Utu na I Wish wa Kusah.

Kupitia ukarasa wake wa Twitter, Maua Sama ameandika; “Kwani ikitokea hujaimba Amapiano unaweza kufutiwa cheti cha usajili Basata au utapokonywa Nida na passport?

“Nipo zangu sehemu hapa nakunywa soda nasikiliza Zai, Utu na I Wish (on repeat) nipo airport njooni mnipige…”

Kufuatia maelezo hayo ya Maua ndipo King Kiba akamjibu; “Hakuna wa kukupiga Zai wangu…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live