Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tunatamani umoja kwa wasanii wa Bongo Fleva" - Mabantu

MABANTU Wasanii wanaounda kubdi la Mabantu

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasanii wanaounda kundi la Mabantu, wamesema wanatamani sana ushirikiano uliopo baina ya wasanii wa mataifa mengine kwa kpeana sapoti katika shughuli zao mbali mbali mfano wasanii wa Nigeria.

Mabantu wamezungumza hayo walipokuwa wakifanya mahojiano na kipindi cha "Empire" kinachorushwa na kituo cha Redio cha E-fm.

"Tunatamani kuona tunabebana na kusogezana kama wenzetu wanavyofanya kitu ambacho tumekuwa tukilalamikia chini chini, kuna vitu huwa tunatamani kufanya, tusingoje hata kaka zetu wafanye" amesema mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo twaah mabantu

Mabantu ni miongoni mwa wasanii ambao wanshiriki ama kutoa sapoti katika kazi za wasanii wenzao kama vile Marioo, Nandy, Young Lunya na wengine wengi.

Mabantu wameshafanya hit song kadhaa kama vile No stress, mwenye nyumba nk

Chanzo: www.tanzaniaweb.live