Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Marekani zasuka mpango wa pamoja katika Michezo na Sanaa

Unnamed 4 Tanzania na Marekani zasuka mpango wa pamoja katika Michezo na Sanaa

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 jijini Dar es salaam na kujadili masuala mbalimbali ya sekta hiyo ikiwa ni pamoja na ujio wa msanii mashuhuri wa uchoraji, Ashley Collins hapa nchini.

Wakizungumza katika kikao hicho ambacho Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James Rodriguez wamejadili pia ujio wa Timu ya wachezaji nguli wanawake ya mchezo wa kikapu wa ligi ya NBA nchini Marekani hapa nchini ambao watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa mchezo huo.

Mchengerwa amesema viongozi hao wamekubaliana kuendeleza malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi kwenye kuendeleza sekta za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza filamu za hapa nchini za “Swahiliwood” ili ziwe katika kiwango cha kimataifa kama zile za nchini Marekani kwa kupata wataalam ambao watasaidia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada (script).

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee ya kuchezea filamu ambazo zingeweza kuwa bora na kusisitiza kuwa ni adhma ya serikali kujenga mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuangalia kodi mbalimbali ili kuwavutia wageni kuja kurekodia hapa nchini.

Aidha amesema eneo jingine ambalo limejadiliwa ni pamoja na kutoa mafunzo maalum katika eneo la haki miliki na hakishiriki kwa kazi mbalimbali za wasanii ikiwa ni pamoja na tuzo za muziki na kwa upande mwingine amesema wamejadili namna ya kushirikisha wataalam kwenye program maalum ya kuibua vipaji vya wasanii na wanamichezo ya mtaa kwa mtaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live