Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamasha la Koffi Olomide lasitishwa nchini Kenya

Koffi Lomomide Nguli wa Muziki wa Rhumba Barani Afrika, Koffi Olomide

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tamasha la mwanamuziki nyota barani Afrika Koffi Olomide, lililotarajiwa kufanyika Desemba 11, jijini Nairobi nchini Kenya limekatishwa.

Waandalizi wa tamasha la Kenya wameahidi kurejesha pesa kamili kwa mashabiki waliopata tiketi za onyesho hilo, wakitaja sababu kadhaa za kuhairishwa kwa tamasha hilo.

Wanaharakati kutoka maeneo mbali mbali waliomba onyesho hilo lisiendelee kutokana na sifa ya nguli huyo kuwanyanyasa wanawake.

Mnamo mwaka wa 2019, mwimbaji huyo wa Soukus wa Kongo ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alipatikana na hatia ya ubakaji wa kisheria wa mmoja wa wachezaji wake wa zamani wakati binti huyo akiwa na umri wa miaka 15.

Olomidé alishtakiwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012 kwa ubakaji lakini mashtaka yalipunguzwa.

Amekuwa matatani na sheria mara kadhaa hapo awali kwa kumvamia mmoja wa wachezaji wake, mpiga picha na mtayarishaji wake.

Hivyo kutokana na matendo yake mbali mbali juu ya unyanyasaji wa wanawake, walio wengi wanamuona kama si mtu wa kuigwa katika jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live