Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID awalipua wasanii wa Bongo "Ndiyo maana mnakosa tuzo"

Sugu Tid TID awalipua wasanii wa Bongo

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni muendelezo wa ‘Bongo Flava Honors’ ambayo ni tamasha maalum lililoandaliwa na rapa mkongwe, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa lengo la kuwapa heshima malejendi wa Bongo Flava ambapo shoo ya kwanza alikata utepe Dully Sykes na zamu hii tamasha hilo linamleta jukwaani TID kuja kupewa maua yake Februari 24, 2023.

Akizungumzia tamasha hilo leo Jumatano, Februari 22, 2023 TID amesema hafurahishwi na wasanii wa siku hizi wa Bongo Flava katika utendaji wao kwani hawautendei haki mziki wa Tanzania.

“Vijana wamebadilisha kabisa muziki wetu hata sauti, wengi wanaimba muziki wa Nigeria ama Sauzi, ‘Amapiano’ lakini ukiangali ‘orijino’ yake sio Tanzania mwisho wa siku tunapoteza uhalisia wa muziki wetu.

“Anachokifanya Sugu kuwaleta wakongwe jukwaani ni kurejesha muziki wetu kwenye hadhi yake, kuufanya muziki uwe laivu, kuwakumbusha watu kwamba muziki wetu umetoka mbali na kuna watu ambao wametumia nguvu na akili yao kuufikisha hapo ulipo leo.

“Muziki wetu bado ni mchanga, ni miaka 20 tu iliyopita ndipo tulianzisha Bongo Fleva na sisi sote ni kizazi cha Bongo Fleva.

Bongo kuna u-fake mwingi sana, hii inafanya muziki wetu unadharaulika mpaka tunakosa tuzo za kimataifa kwa sababu sisi tunachukua vitu vya watu tunaacha vya kwetu, Umarekani ni mwingi, hii mbaya sana. Sisi Tanzania tunapoteza muziki wetu na uhalisia wake,” amesema Sugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live