Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TID Alia na Bongo Kukosa Tuzo Zake za Muziki

Mwanamuziki TID TID Alia na Bongo Kukosa Tuzo Zake za Muziki

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSANII nguli wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed 'TID' ametoa sababu zake kuhusu muziki wa Bongo Fleva kutosikika kama zamani na badala yake muziki wa nje ndio unasikika zaidi Tanzania.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, Mnyama amesema; "Uzalendo ni kitu muhimu sana na tukizungumzia uzalendo lazima tuwe na uthamani wa kujali kitu gani amabcho tumefanya.

"Kitu ambacho kinatuangusha sisi kuona miziki mingine inatuchukua sisi ni kwa sababu hatuna hata awards (tuzo) zetu. Tuzo zinafanya kwanza muziki unakuwa na heshima kwa sababu pale ndio kipimo pekee cha kusema muziki wa Tanzania huu hapa na tunajadili nani kafanya vizuri kwenye kila kipengele,'' amesema TID.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live