Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Super Nyamwela anavyopambana na Ubuntu Band

55626 Pic+nyamwela

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mnenguaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini aliyejipatia umaarufu akiwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta, Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’, ameendelea kutamba katika medani hiyo ya unenguaji kwa kuanzisha bendi yake inayojulikana kwa jina la Ubuntu Traditional.

Nyamwela ambaye wiki iliyopita ametoa wimbo ‘Aisha’ amezungumza na Starehe akisema bendi ya Ubuntu ambayo hutumbuiza nyimbo za asili pekee, mpaka sasa ina miaka mitano toka aianzishe.

Akizungumzia maendeleo yake amesema ameshafanya ziara katika nchi za Japan, Qatar, UAE na Nigeria kuanzia mwaka 2017.

Anasema lengo la bendi yake ni kufanya bendi iwe ya kimataifa na hapa Tanzania wawe wanafanya kazi kuanzia Serikalini na kwenye matamasha makubwa.

Nyamwela ambaye amekuwa tofauti na wanenguaji wengine hapa nchini kutokana na kupenda kujibidiisha katika fani yake , huku akibebwa zaidi na ubunifu wa staili za unenguaji.

Pia, anasema wimbo wa Aisha hakutunga mwenyewe bali wamechangia aidia watu wa tano ndio wakapata jina la Aisha.

Aelezea kwa nini makundi ya Asili ya zamani yamekufa

“Ni kweli kabisa makundi ya nyimbo za asili yalifanya kazi nzuri sana kuwakilisha muziki wetu wa asili kimataifa ,ila naona walipotea kwa sababu wengi wao walioa wanawake Wakizungu nje ya nchi.”

“Mimi nimeyaona hayo makosa ndio maana mpaka nimeamua kuweka Ubuntu ili watu waijue na nimesha jifunza mengi kutoka kwa walio nitangulia huko nyuma”

Kwa nini Ubuntu?

Nyamwela aliwahi kutoa albamu binafsi Master of the Tample na Kilomdoko.

“Yeah ni kweli kabla Ubuntu nilikuwa albamu mbili, lakini Ubuntu ndio ilikuwa ndoto yangu ,nilitamani kuiona siku na mimi ni miliki bendi yangu mwenyewe, ila isifanane na nyingine nilizoweza kupitia kwenye maisha yote ya muzuki.”

Anaweza kukimbizana na Dunia ya sasa ya muziki wa kizazi kipya?

Kutokana na muziki wa kizazi kipya na Nyamwela anafanya muziki wa Asili,anasema anatengeneza fedha kwa kuwa hakuna ushindani mkubwa.

“Naona natengeneza pesa nyingi kuliko hao wana muziki wa kizazi kipya, kwa sababu mimi nikifanya shoo zangu za nje tatu nina uhakika wakuendesha maisha yanga bila kupiga shoo hapa Tanzania na nikipiga shoo hapa Tanzania kwenye hoteli tu kwa wiki ninapesa nyingi mno kuliko hao.”

Soko la muziki asilia likoje?

“Soko kiukweli hapa Tanzania ni bado linachangamoto kidogo ila nimejipanga vizuri kukubaliana nayo, na mimi malengo yangu kufanya shoo kwenye mahotel makubwa na kufanya kazi mashirika tofauti ya kiserekali na binafsi, “Niligundua wasani wengi muziki wa asili wanaukimbia kwa sababu wanaona haulipi ila kwangu mimi naona unalipa sana tena zaidi sana tofauti na muziki niliowahi kufanya miaka yote takribani miaka 30 kwenye ‘game.’’



Chanzo: mwananchi.co.tz