Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Summer Walker amjia juu baba mtoto wake kwa kudai amehusika kwenye album yake

Summer Walker London On Da Track Summer Walker amjia juu baba mtoto wake kwa kudai amehusika kwenye album yake

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kama mwimbaji Summer Walker bado ana hasira sana juu ya mzazi mwenzake producer London On Da Track baada ya kusema amehusika kwa asilimua kubwa kuiandaa album ya Summer.

Siku ya Ijumaa, mwimbaji huyo wa R&B aliachia albamu yake ya pili Still Over It, ambayo ina nyimbo zilizoandikwa na kutayarishwa na mpenzi wake wa zamani, ambaye pia alimvutia muziki wake mpya.

London, ambaye ametajwa kuandika nyimbo tisa zikiwemo "Bitter," "Ex for a Reason," na "Throw It Away," alirepost ujumbe wa shabiki ambaye alionesha jinsi gani mtayarisha huyo amehusika kwenye uandaaji wa maudhui ya albamu kupitia Instagram.

"London on Da Track, ni mtu wa kwanza kulipwa kutoka kwenye album ambayo katukanwa japo kaiandaa mwenyewe" Ulisomeka ujumbe huo.

Baada ya ujumbe huo, Summer Walker alikuja kujibu kuwa mtayarishaji huyo ambaye pia ni baba wa mtoto wake hajaandika wala kutayarisha chochote kwenye album yake.

"Hajaandika wala hajatayarisha chochote humu, alikua anachagua tu watu wakufanya nao kazi na kufanya uzinzi na wanawake wakati nikiwa mjamzito." amejibu Summer.

View this post on Instagram

A post shared by The Shade Room (@theshaderoom)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live