Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu adokeza ujio wake mpya Kwenye Bongo Flavour

IMG 20220123 WA0035 1 Sugu

Sun, 23 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ukimya wa zaidi miaka mitano mfululizo, akiwa nje ya sanaa ya muziki, hatimaye mwanamuziki nguli wa Hip hop nchini, Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ amewataarifu mashabiki na wapenzi wa kazi zake juu ya ujio wake mpya ifikapo Februari 14, 2022.

Kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram ambapo Sugu ameandika,

“Too much PRESSURE, wengine wanasema itoke fasta hata audio, wengine wanasema tusubiri video, naomba mnivumilie kidogo tufanye mambo mazuri, maana mmesubiri ngoma mpya kwa miaka 6 sasa, so ni vema tuwe na a proper comeback… Sasa expected WORLD PREMIER ni FEB. 14

Chanzo: www.tanzaniaweb.live