Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu: Ana miaka chini ya 18 ni historia ya binti nilikutana naye usiku

Sugu 2 Pic Data Msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ameimba wimbo wa kwanza wa Ana miaka chini ya 18 kwenye The Dream Concert huku akieleza ni wimbo ambao aliutunga baada ya kukutana na binti akifanya kazi za usiku.

"Nilikutana naye nikamuuliza una umri gani, akasema miaka 17, nikamuuliza kwanini uko hapa? Historia aliyonipa ndiyo ilinisukuma niandike wimbo huu," amesema Sugu.

Huo ndio ulikuwa wimbo wa kwanza wa Sugu kuimba kwenye Dream Concert, tamasha maalumu la mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini la kuadhimisha miaka 30 ya muziki wake lililofanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Juni Mosi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Akisikilizwa na wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo akiwamo mgeni rasmi, Rais Samia Suluhu Hassan, Sugu amesema safari ya muziki kwake ilikuwa na changamoto.

"Sina chuki na wadogo zangu ambao wanapiga pesa kwenye muziki sasa, kwani hata mimi sija lost, bado mimi ni taita," amesema Sugu katika tamasha hilo.

Mtoto wa Dandu, Ruge wakumbukwa Dream Concert

Wadau wa Muziki wakiongozwa na Rais Samia wamesimama kwa muda kuwakumbuka wa wasanii na wadau wa muziki nchini waliotangulia mbele za haki.

Tukio hilo limefanyika kwenye tamasha hilo la The Dream Concert huku wakiwakumbuka Ruge Mtahaba aliyetangulia mbele za haki, Cool James 'mtoto wa Dandu' Mr Ebbo, Adili Kumbuka, Ranga, Cpwaa, John Walker na Complex ambao walitajwa kama wadau wakubwa wa muziki nchini huku picha zao na vipande vya baadhi ya nyimbo zao zikionekana kwenye skrini kubwa ndani ya ukumbi wa Serena linapofanyika tamasha hilo.

Pia, tamasha hilo limetumika kumuombea mwanamuziki na mbuge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule 'Profesa Jay' ambaye anaumwa kwa muda sasa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz