Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole kaingia studio na msanii huyu mkubwa Afrika

B1ff82a3bbb3a95f29254133373325f0 Msanii wa Bongo Flava

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema yupo katika mazungumzo na msanii mkubwa Afrika kwa ajili ya kushirikiana naye kutoa ngoma moja kabla ya mwaka 2021 kupita.

Akizungumza na gazeti hili msanii huyo alisema kwa sasa hawezi kumtaja msanii huyo, lakini ni kutoka Afrika na afanya vizuri kwenye tasnia ya muziki.

“Nataka kufanya kitu cha tofauti kidogo kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wakubwa hapa nchini, akiwemo Naseeb Abdul ‘Diamond’ ndio maana niko kwenye mazungumzo na msanii huyo mkubwa kwa ajili ya kufanya naye kolabo,” alisema Shilole.

Msanii huyo alisema mazungumzo yao yanakwenda vizuri na muda siyo mrefu ataanza harakati za kuandaa mashairi kabla ya kumfuata nchini kwake au yeye aje Tanzania kwa ajili ya kuweka sauti na kutengenezea Video yake.

Alisema mipango yake ni kutoa audio na video lengo ni kuwapa mashabiki wake ladha tofauti na kufurahia muziki wake ambao ndio uliompa umaarufu na mafanikio aliyokuwa nayo hivi sasa. Shilole ni mmoja wa wasanii ambao

Chanzo: www.habarileo.co.tz