Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole "apiga" watu mitandaoni

Shishi Baby.jpeg Shilole

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na Mjasiriamali Zena Yusuf Mohammed "Shilole" amekemea kitendo cha watu wasiofahamika katika mitandao ya kijamii kutumia jina lake na kufanya utapeli.

Tangazo hilo lililotolewa katika mtandao wakijamii wa Facebook lililokuwa linatangaza nafasi za kazi na hatimaye waombaji wanaombwa hela ili kupewa nafasi hiyo ya kazi.

Shilole amelazimika kuwajuza mashabiki wake wote kuwa hahusiki na akaunti yoyote katika mtandao wa Facebook wala hajatangaza nafasi ya kazi sehemu yoyote.

Shilole anasema kuwa, kwa taarifa zozote kuhusu habari zake atatoa kupitia katika ukurasa wake rasmi wa Instagram ambao una tiki ya bluu (Verified).

Shilole ameandika; “Nasikitika sana kwa watu ambao wanatumia vibaya mitandao, pamoja na jina langu kwa lengo la kuwatapeli wengine.

“Kwa sasa sijatangaza nafasi yeyote ya kazi, na ukurasa huo sio wangu. Swala lolote linalotoka kwangu litaonekana kwenye kurasa zangu rasmi, hapa Instagram ni @officialshilole na Facebook ni Shilole na account zote ziko verified (zina kitiki cha bluu). Hivyo usikubali kudanganyika na watu wote wanaotumia jina langu isivyo halali"

“Nitafuatilia kwa ukaribu ili sheria na vyombo husika viweze kuchukua hatua.” ameandika Shilole katika mtandao wake wa Instagram

Chanzo: www.tanzaniaweb.live