Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga marufuku wasanii kutumbuiza wanafunzi Shuleni

Shoo Shulee.jpeg Serikali yapiga marufuku wasanii kutumbuiza wanafunzi Shuleni

Sat, 6 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Elimu na Michezo Uganda imepiga marufuku mara moja kwa shughuli zozote zinazohusiana na wanamuziki kutumbuiza wanafunzi katika Shule za Msingi na Sekondari.

Marufuku hiyo ambayo inaanza kutumika mara moja itatekelezwa katika shule za msingi na sekondari za serikali na za kibinafsi.

Haya yamo katika waraka ambao ulitolewa kwa walimu wakuu na Wakuu wote wa shule na Dk Jane Okou kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara.

"Walimu wakuu na Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari wanaonywa kutoajiri au kuruhusu yeyote kati ya "wasanii" hawa kufanya maonyesho shuleni. Wasimamizi wa shule wanapaswa kuwajibika na kudii maagizo haya, yule ambaye atapatikana kuenda kinyume na hii maagizo atachukuliwa hatua'' Agizo kutoka katika waraka hiyo.

Wizara pia ilibainisha kuwa shughuli za ziada shuleni kwa kawaida kama vile michezo na uimbaji, vilabu vya mijadala, n.k na ikiwa shule zinahitaji kujiliwaza, basi zinaweza kushiriki katika maigizo ya kuigiza au kupanga matamasha.

Haya yanajiri baada ya mwezi uliopita Mbunge wa Tororo Sarah Acheing Opendi kuliambia bunge kuwa kiwango cha wanamuziki kueneza uasherati shuleni ni cha kutisha na hivyo akatoa wito wa kupigwa marufuku kwa wanamuziki wa kilimwengu kutumbuiza shuleni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live