Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruger atua Bongo, amtia dongo Kizz Daniel "Sijasahau begi"

Ruger2 Ruger atua Bongo, amtia dongo Kizz Daniel

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Afrobeat barani Afrika kutokea nchini Nigeria, Michael Adebayo Olayinka maarufu kama Ruger ametua nchini Tanzania jana Jumatano, Septemba 28, 2022.

Ruger ametua Tanzania akitokea London, Uingereza ambapo anatarajia kutumbuiza jumamosi hii Oktoba 1 katika ukumbi wa Ware House uliopo maeneo ya Masaki, Dar es Salaam.

Ujumbe wa msanii Ruger baada ya kutua Tanzania kwa mara ya kwanza; "Tanzania nipo hapa na sijasahau mabegi yangu, tukutane Oktoba 1," ameandika Ruger kwenye akaunti yake ya Twitter.

Ikumbukwe kuwa, mwezi uliopita mkali wa muziki Nigeria, Kizz Daniel aligoma kutumbuiza jijini Dar es Salaam licha ya kulipwa akidai kuwa amesahau begi la nguo zake Nairobi nchini Kenya.

Wasanii wengine watakaopanda jukwaa moja na Ruger ni mkali wa bongo fleva Jay Melody pamoja Nyashinski kutokea nchini Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live