Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruby atamani kifo

IMG 20220410 WA0011 Ujumbe wa Ruby

Mon, 11 Apr 2022 Chanzo: dar24.com

Msanii wa Muziki Ruby, hii leo amezua taharuki kote mitandaoni muda mfupi baada ya kuweka chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akiashiria kuwa anapitia wakati mgumu kwenye maisha yake kiasi cha kutamani kufa.

“Najisikia tu nife nikapumzike na ya dunia.” Ameandika Ruby.

Aidha kufuatia ujumbe huo uliowashtua watu mbali mbali, mwanamitindo maarufu nchini Flaviana Matata ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kutoa rai kwa yeyote aliyekaribu na Ruby kuhakikisha anampatia msaada ili kuepuka athari zaidi.

“Yeyote aliyekaribu na Ruby anapaswa kuhakikisha anapata msaada kabla ya kuchelewa. Tafadhali” ameandika Matata.

Mpaka sasa haijajulikana ni nini kinachomsibu Ruby.

Chanzo: dar24.com