Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rosa Ree: Nimeamua kumiliki muziki wangu mwenyewe

Cxeg Rosa Ree Rosa Ree

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa @rosa_ree ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya iitwayo "Goddess" ambayo ameitaja kuiandaa kwa takribani miaka minne. Ameeleza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye maelezo yake pia @rosa_ree amebainisha kwamba, anaachia album yake hiyo kama msanii anayejitegemea mwenyewe yani adhaminiwi na lebo yoyote na wala hajauza muziki wake kwa kampuni yoyote ya usambazaji wa muziki.

Ameeleza kampuni nyingi zilimfuata kutaka kumdhamini lakini amesema amechagua kumiliki muziki wake kwa asilimia mia.

Kuhusu album yake, @rosa_ree ameeleza kwamba ameweka kila version ya Rosa Ree kwenye album hiyo;

"ROSARY the Daughter, ROSAA the Sister/Friend, ROSARY the Mother, ROSA REE the Artist na hata yule Rosa Ree nisiyemjua ambaye bado naendelea kumgundua" - ameeleza na kuongeza, "Nimewapa MIMI HALISI. I’ve put my blood, sweat and tears into this album."

Kaa tayari kwa album hii mpya na ya kwanza kwa @rosa_ree katika safari yake ya muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live