Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rosa Ree: Kuvishwa pete hakunifanyi niache muziki

B3c6683e24e5905c820f87c7908bef1a Rosa Ree akivishwa pete

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mrembo anayefanya vizuri katika muziki wa Hip Hop, Rosary Robert 'Rose Ree' amesema kitendo cha kuvalishwa pete na mchumba wake anayefahamika kama ‘King’ hakijaja mapema na kwa sababu hiyo haimfanyi kuacha muziki.

Rosa Ree amesema ametoka mbali na mpenzi wake huyo hata hivyo wamepanga kufanya mambo mengi zaidi kwenye maisha yao.

"Wapo ambao watasema mimi bado ni Mdogo? Lakini naamini kwamba pale unapokuwa na nguvu ndio muda mzuri wa kupanga malengo yako, napenda muziki tangu nikiwa mdogo hadi sasa hivyo hata nikiwa mzee ntaendelea Kuupenda'' amesema Rosa Ree.

"Ukisema muziki ufanye nisifanye maisha mengine haitakua sawa, kwaiyo ukisema nikifika miaka hamsini ndio nianze kutafuta mwenza itakua uongo," ameongeza Rosa Ree. Aidha ameendelea kuwaomba mashabiki kusapoti muziki wake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz