Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma: Bongo Fleva haijulikani Marekani

Roma Roma: Bongo Fleva haijulikani Marekani

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki maarufu wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania Roma Mkatoliki ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani amevunja ukimya kuhusu maendeleo ya sanaa ya muziki wa bongo fleva ughaibuni hasa nchini Marekani kwa madai ya kuwa muziki huo hajulikani kabisa.

Roma ameonesha kushangazwa na kudorora kwa makuzi ya muziki huo nchini humo ukilinganisha na muziki wa mataifa mengine ya afrika ambayo walau yanapata nafasi.

"Shida ya huku tulipo, huwezi kwenda sehemu ya Starehe (Club) ukakuta ngoma za Bongo flava hata 2 tu zinapigwa, kuna muda unatamani uende Disco ukacheze hata Singeli lakini wapi!,

Kinyonge mnarudi magetoni mna-connect Bluetooth Speaker mnasikiliza Wana! SEMA IPO SIKU TU WATAIJUA BONGOFLEVA." Ameandika.

Roma ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter huku akihitimisha kwa kudhihirisha kuwa bado anamatumaini ya kuwa upo wakati muziki huo utafikia katika hatua ya kufahamika nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live