Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rich Mavoko aachia "Fundi"

IMG 20220325 WA0030 Rich Movoko

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: dar24.com

Mwaka 2022 umeingia na kifurushi cha burudani kwa wapenzi wa muziki wa bongo feva, kutokana na wasanii mbali mbali kuachia kazi zao kwa mfululizo kiasi cha kuifanya tasnia kuchangamka.

‘Messi wa bongo fleva’, Rich Mavoko hatimaye naye ameiachia rasmi album yake mpya iitwayo ‘FUNDI’ ambayo mpaka sasa tayari ameieneza kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikìliza na kupakua muziki Online.

Mavoko ametimiza ahadi yake kwa mashabiki waliokuwa wakisubiri kwa hamu ujio wa album hiyo iliyokuwa itokea mapema  tangu wiki moja iliyopita na baadae kuahirishwa ili kupisha shughuli za maombolezo ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Album hiyo ina jumla ya nyimbo kumi na sita ambazo saba kati ya hizo ameshirikiana na wasanii wengine kadhaa akiwamo Masauti kutika nchini Kenya, Fid Q, Nviir, H art the band,  Big Zulu na Ssaru pamoja na msanii chipukizi anayefanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Saraphina Michael.

Chanzo: dar24.com