Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rich Mavoko Afunguka Kujiunga Kings Music

Mavoko3 Mavoko

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Richard Martin almaarufu Rich Mavoko amefunguka kuhusiana na madai yanayoendelea mitandaoni hivi sasa kuwa huwenda akajiunga katika Lebo ya Kings Music yake mtu mzima, King Kiba.

Rich Mavoko ambaye awali alikuwa kwenye Lebo ya Wasafi chini ya Diamond Platnumz anasema kuwa, watu wawe wapole kwa sababu kila jambo lina wakati wake.

“Mimi kujiunga na Lebo ya Kings Music naomba kwanza mashabiki wangu wawe wapole kwa sababu kama kweli hiyo ishu ipo, basi watajua, sitawaficha chochote,” anasema Rich Mavoko ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya ya Sio Leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live