Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny atangaza ujio wa tamasha la Mac Voice

Tamasha Tamasha la Mac Voice liko mbioni

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka WCB Wasafi Raymond Shaban maarufu Rayvanny ameweka wazi taarifa za ujio wa ziara ya tamasha maalumu kwa ajili ya msanii wake mpya kutoka kwenye Lebal yake Next Level Music.

Rayvanny amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa instagram (insta story) kwa kuandika maneno yenye kusomeka “Macvoice Tour.. Show Time”, maneno yenye kuashiria kuwa wasaa wa msanii huyo kuanza ziara yake ya kwanza tangu kutambulishwa kwake inaelekea kuanza rasmi.

Mac Voice ni msanii mpya na wa kwanza kutambulishwa chini ya Lebal ya muziki inayomilikiwa na msanii Rayvanny takribani mwezi mmoja uliopita akiachia Extended Playlist (EP) iitwayo “Voice” yenye jumla ya nyimbo sita.

Ambaye hivi karibuni pia ametajwa kuwania tuzo ya African Entertainment Awards USA 2021, kupitia kipengele cha msanii bora anayechipukia kwa mwaka 2021 akishindana vikali na wasanii wengine kutoka nchi kadhaa barani Afrika akiwemo Oxlade, Liya Guchi, Ayra Starr na Omah Lay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live