Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny: Sijapoteza kitu WCB

Rayvanny Tequ Rayvanny

Sun, 17 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni siku chache baada ya kufunguka kuondoka WCB, mkali wa mashairi ya mapenzi, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema amefanya kila alichokuwa anakitaka ndani ya lebo hilo ndio sababu kubwa iliyomfanya aondoke na kupisha wengine wapate fursa.

Rayvanny amemshukuru Diamond kwa fursa aliyompa  na kumfungulia miango ya kuwa msanii wa kwanza kutwaa tuzo kubwa ya BET, hivyo anatamani kuona wasanii wengine wanapata fursa kama yake huku naye akitafuta namna ya kuwasaidia wasanii wanaochipukia nje ya WCB.

Vanny Boy alisema: “Ndani ya miaka sita niliyoishi WCB sina nilichokipoteza nimekuwa mkubwa nataka kutumia nafasi hii nami kukuza wengine kupitia lebo yangu ya Next Level Music. Ninaamini nilichojifunza kule nitakitumia kuwatoa wengine kufikia ndoto zao.”

“Namshukuru kaka yangu na bosi wangu Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kunijenga na kunifanya kuwa mkubwa ninayetamani kupitia ndoto zake za kusaidia watu nami niweze kuwafanya wasanii kuweza kukua na kuitambulisha sanaa ya muziki ndani na nje ya nchi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live