Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rayvanny: Nimekua kimuziki tangu niondoke WCB

DEC0BF66 B7E0 49E3 8421 F6C6CFFA4C5E.jpeg CEO wa Next Level Music, Rayvanny

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema tangu aondoke kwenye lebo ya WCB amejihisi kukua kimuziki na kwa sasa anawaza mambo makubwa zaidi.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo, amesema changamoto anazokutana nazo pamoja na ushindani uliopo kwenye gemu ya bongo fleva, vimemkomaza zaidi.

“Ukweli sijutii maamuzi yangu, zaidi napambana ili niweze kuwa mkubwa zaidi, sababu huku kila kitu wakuulizwa ni mimi na sababu ndiyo bosi mkubwa ninayehusika na mambo yote ikiwemo kulipa wasanii na mengineyo,” amesema.

Aidha, amesema kwa jinsi anavyofanya vizuri katika gemu hiyo, anaamini mpaka kufikia mwaka ujao atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini na wenye wafuasi wengi kuliko ilivyo hivi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live